Taarifa za Jumla

Taarifa za Jumla

Ufafanuzi wa Istilahi

Ndege Inayodhibitiwa kwa Mbali (Remotely Piloted Aircraft — RPA)

Ndege isiyo na rubani ndani yake, ambayo huendeshwa na rubani kutoka kituo cha udhibiti wa mbali.

Mfumo wa Ndege Inayodhibitiwa kwa Mbali (Remotely Piloted Aircraft System — RPAS)

Mfumo unaojumuisha ndege inayodhibitiwa kwa mbali, kituo au vituo vyake vya udhibiti wa mbali, viunganishi vinavyohitajika vya amri na udhibiti, pamoja na vipengele vingine vyovyote vilivyoainishwa katika usanifu wa aina husika ya mfumo.

Rubani wa Mbali (Remote Pilot)

Mtu anayewajibika kuendesha vidhibiti vya urubani vya ndege inayodhibitiwa kwa mbali wakati wa safari ya ndege.

Rubani Mkuu wa Mbali (Remote Pilot-in-Command)

Rubani wa mbali aliyeteuliwa kuwa msimamizi mkuu wa safari ya ndege na anayewajibika kuhakikisha safari hiyo inaendeshwa kwa usalama.

Kituo cha Rubani wa Mbali (Remote Pilot Station)

Sehemu ya mfumo wa ndege inayodhibitiwa kwa mbali (RPAS) yenye vifaa vinavyotumika kuendeshea ndege hiyo.

Tafadhali hakiki ufafanuzi huu kwa kuulinganisha na Kanuni za Usafiri wa Anga (Mifumo ya Ndege Zinazodhibitiwa kwa Mbali), za mwaka 2026, na ufanye marekebisho yanayohitajika ili kuhakikisha usahihi na uthabiti wa istilahi kabla ya kuchapishwa. [IA1.1]

Droni Nchini Tanzania

Unapanga kuleta, kununua, kusajili au kuendesha droni nchini Tanzania? Mwongozo huu unaeleza hatua za kuzingatia, nyaraka unazoweza kuhitaji na mahali pa kuanzia maombi yako kupitia Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), kwa kutumia Mfumo wa Huduma za Usafiri wa Anga (Civil Aviation Services Portal — CASP).

  • Ninatembelea Tanzania na nina droni.
  • Ninaishi Tanzania na ninataka kutumia droni.
  • Ninaagiza au ninauza droni.
  • Taasisi yangu inataka kuendesha droni.
  • Ninataka kufahamu maeneo ninayoruhusiwa kurusha droni.
  • Ninahitaji taarifa kuhusu mafunzo au umahiri wa urubani.
  • Ninahitaji kanuni, fomu au viwango vya ada.
  • Ninaendesha ndege droni kwa burudani au ninataka kujiunga na klabu ya droni.
  • Ninawakilisha serikali, utafiti au taasisi ya elimu.
  • Ninataka kutoa taarifa ya droni, ajali au tukio la kiusalama.

Muhimu: Usilete droni nchini Tanzania wala kuanza kuiendesha kabla ya kuthibitishwa na kupata vibali vyote vinavyohitajika. Kumbuka kwamba kumiliki droni, kuisajili au kuwasilisha maombi ya droni hakukupi uhalali wa au ruhusa ya kufanya kila safari ya droni.

Mambo Matatu Ambayo Kila Mtu Anapaswa Kuyafahamu

  • Kila droni inayoendeshwa nchini Tanzania lazima isajiliwe na TCAA, na kila safari ya ndege lazima iwe na idhini inayofaa kutoka TCAA. Kumiliki droni au kuwa umewasilisha maombi hakukupi uhalali au ruhusa ya kufanya kila safari ya droni.
  • Pata vibali vyako kabla ya kusafiri au kuendesha droni. Droni inayowasili bila kibali cha uingizaji kutoka TCAA au bila usajili unaohitajika, inaweza kutaifishwa katika eneo la kuingilia nchini.
  • Zingatia kanuni za usalama katika kila safari ya droni: usipande juu ya mita 120 (futi 400), iweke droni ndani ya upeo wa macho yako, kaa mbali na watu, viwanja vya ndege na maeneo yenye vizuizi na heshimu faragha.

Imesasishwa mwisho: 20 Oct 2026

Unahitaji Msaada?