Mamlaka inapenda kuwataarifu watumishi wa umma na watumishi wa sekta binafsi wanaofanya kazi katika sekta ya usafiri wa anga kuhusu fursa ya kuomba kujiunga katika Programu ya Ushirika ya ROK–KAU 2026 kuhusu Sera za Kimataifa za Usafiri wa Anga (Korea Fellowship Programme on Global Aviation Policy), ambayo ni programu ya mafunzo ya uzamili ya kimataifa iliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Anga cha Korea (Korea Aerospace University) kwa ushirikiano na Serikali ya Jamhuri ya Korea.