WAZIRI MBARAWA ARIDHISHWA NA MAENDELEO YA UJENZI W...

WAZIRI MBARAWA ARIDHISHWA NA MAENDELEO YA UJENZI WA MIUNDOMBINU MIPYA YA CATC

31 August, 2026
WAZIRI MBARAWA ARIDHISHWA NA MAENDELEO YA UJENZI WA MIUNDOMBINU MIPYA YA CATC

Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Prof. Makame Mbarawa (Mb), ametembelea na kukagua ujenzi wa miundombinu mipya ya Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) kinachojengwa Banana, Dar es Salaam, na kueleza kuridhishwa na maendeleo ya mradi huo.

Mhe. Waziri Mbarawa alipokewa na mwenyeji wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Dkt. Jabiri Bakari, ambaye alimhakikishia Mhe Waziri kuwa mradi huo utakamilika kwa wakati, Dkt .Bakari aliambatana pamoja na Menejimenti ya TCAA.

Akizungumzia baada ya kutembelea mradi huo jijini Dar es Salaam, 23 Julai 2026, Mhe. Waziri Mbarawa alisema mpaka sasa mradi huo  umefikia asilimia 23.9 ya utekelezaji ikiwa ni miezi 11 tangu kuanza kwa mradi. 

Mradi huo wenye thamani ya takribani shilingi bilioni 78 unalenga kuwezesha upatikanaji wa miundombinu ya kisasa ya mafunzo ya usafiri wa anga na kuimarisha nafasi ya Tanzania kuwa kitovu cha mafunzo ya usafiri wa anga barani Afrika. 
Mhe. Prof. Mbarawa ameipongeza TCAA kwa usimamizi wa mradi.

Need any help?