Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Dkt. Jabiri K. Bakari, amekutana na Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO), Dkt. Agnes Kijazi, tarehe 12 Juni 2026, katika ziara ya kikazi iliyolenga kujadili ushirikiano katika huduma za hali ya hewa na sekta ya usafiri wa anga.
Mazungumzo yalisisitiza umuhimu wa kuimarisha uwezo wa huduma za hali ya hewa, kuendeleza ushirikiano kati ya WMO na TCAA, pamoja na kuharakisha matumizi ya mifumo ya kidijitali ili kuimarisha usalama wa anga na maendeleo endelevu. Dkt. Kijazi aliambatana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dkt. Ladislaus Chang’a, na Bw. Emmanuel Tumaini Kibebwana, Meneja wa Teknolojia ya Habari (IT).