Kuhusu TCAA

Mamlaka ya Usafiri wa Anga ni chombo cha serikali kinachosimamia na kudhibiti sekta ya usafiri anga (huduma za usafiri wa anga +  huduma za viwanja vya ndege) na kutoa huduma za uongozaji ndege nchini Tanzania, ilianzishwa chini ya Sheria ya Usafiri wa Anga, Sura. 80. Mamlaka inatekeleza jukumu muhimu katika kuhakikisha kuwa mfumo mwafaka wa usafiri wa anga unaanzishwa na kudumishwa ili kusaidia maendeleo ya nchi. Dhamira ya Mamlaka ni kuhakikisha usalama, ulinzi na uendeshaji wenye utaratibu wa usafiri wa anga nchini Tanzania kupitia usimamizi madhubuti, utoaji wa huduma bora za uongozaji ndege na mafunzo wakati huohuo tukidumisha ubora, kulinda mazingira na kuhifadhi maslahi ya wadau.

Unahitaji Msaada?