Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (Tanzania Civil Aviation Authority – TCAA) ni taasisi ya umma yenye hadhi ya kisheria iliyoanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Usafiri wa Anga, Sura ya 80 (Marekebisho ya mwaka 2023).
Mpango Mkakati huu umeandaliwa kwa kuzingatia Mwongozo wa Mpango Mkakati wa Muda wa Kati na Bajeti wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na umebainisha masuala yote ya kimkakati yanayotarajiwa kutekelezwa katika kipindi cha miaka mitano (05) kuanzia mwaka wa fedha 2021/22 hadi 2025/26.
Maandalizi ya Mpango Mkakati huu yametokana na mapitio ya Mpango Mkakati uliopita wa mwaka 2016/17 hadi 2020/21. Mapitio hayo yamezingatia mipango mbalimbali, mabadiliko yaliyojitokeza katika sekta ya usafiri wa anga, changamoto zilizobainika pamoja na mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji wa mpango uliopita, na uchambuzi wake umejumuishwa katika mpango mpya.