Usanifu wa taratibu zinazowezesha Ndege kutumia Mifumo yake Kutua
Huduma ya usanifu wa taratibu zinazowezesha ndege kutumia mifumo yake kutua (IFPD) hutengeneza taratibu za kiwango cha kimataifa zinazozingatia viwango vya ICAO ili kuimarisha usalama wa safari za anga, kuongeza uwezo wa matumizi ya anga, na kupunguza athari za mazingira.
Kwa kutumia programu za kisasa za usanifu wa taratibu za ndege pamoja na timu ya wataalamu wenye uzoefu na vyeti vinavyotambulika katika taaluma hii, tunatoa huduma za usanifu wa taratibu za ndege zenye usahihi wa hali ya juu na zinazotegemea uchambuzi wa kina wa takwimu. Huduma hizi hutolewa ndani ya anga la Tanzania na pia kwa nchi nyingine zinazohitaji utaalamu wetu. Tunabuni, kuhuisha, kuthibitisha na kusimamia aina zote za taratibu za ndege katika hatua mbalimbali za safari za ndege.
Wigo wa huduma zetu unajumuisha:
- Taratibu za ndege kutua zisizo na usahihi wa juu.
- Taratibu za ndege kutua zenye mwongozo wa wima
- Taratibu za ndege kutua zenye usahihi wa juu.
- Njia maalumu za kuondoka kwa ndege
- Njia maalumu za kuwasili kwa ndege
- Taratibu za kuendesha ndege kwa kuona
- Njia za ndege angani
- Utengaji na Uanishaji wa maeneo na kanda za uongozaji ndege
Aidha, tunatoa huduma za uchambuzi wa awali wa taarifa za vizuizi, utayarishaji wa ramani za uongozaji ndege, uhakiki wa awali wa taratibu za ndege na kuwezesha uchapishaji wa taarifa katika Chapisho Rasmi la Taarifa za Anga (AIP) ili kuhakikisha uzingatiaji wa matakwa ya kisheria na uwiano wa kikanda katika usafiri wa anga.
Iwapo unahitaji kutekeleza taratibu za kisasa za Performance-Based Navigation (PBN) kwa ajili ya kuboresha ufanisi wa eneo la uwanja wa ndege au unahitaji ushirikiano wa kiufundi katika ngazi ya kikanda, timu yetu ya IFPD iko tayari kufanya kazi hiyo kwa usahihi na ubora unaohitajika katika sekta ya kisasa ya usafiri wa anga.
Kwa maombi ya huduma za IFPD, tafadhali wasiliana na:
Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)
S.L.P. 2819
Dar es Salaam, Tanzania
Barua pepe: barua@tcaa.go.tz
Simu: +255 22 2327000