Usajili wa Ndege

Mtu yeyote hataruhusiwa kuendesha ndege yoyote ndani ya au kuruka juu ya eneo la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania isipokuwa ndege inayostahili kusajiliwa iwe imesajiliwa na mmiliki wake kwa mujibu wa Kanuni hizi na Mamlaka iwe imetoa Cheti cha Usajili wa Ndege (Certificate of Registration) kwa ndege hiyo, au ndege hiyo iwe imesajiliwa katika nchi mwanachama wa Mkataba wa Kimataifa wa Usafiri wa Anga wa Chicago (Convention on International Civil Aviation).

Ili kuomba Cheti cha Usajili wa Ndege, tafadhali kamilisha yafuatayo:-

   i. Andika barua kwa Mkurugenzi Mkuu kuomba kibali cha kuingiza ndege kwa ajili ya usajili na uendeshaji ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;

   ii. Jaza na kuwasilisha Fomu TCAA-AC-AWS001B kwa Mkurugenzi Mkuu;

   iii. Lipa ada ya maombi kama ilivyoainishwa katika Waraka wa Taarifa za Anga (Aeronautical Information Circular – AIC).

 

Maelekezo zaidi yanapatikana katika nyaraka zifuatazo za kikanuni

   i. Kanuni za Usafiri wa Anga kuhusu Usajili na Alama za Ndege za mwaka 2017 kama zilivyorekebishwa [Civil Aviation (Aircraft Registration and  Marking) Regulations, 2017];

   ii. Kanuni za Usafiri wa Anga kuhusu Ubora wa Ndege Kuruka za mwaka 2017 kama zilivyorekebishwa [Civil Aviation (Airworthiness) Regulations, 2017];

   iii. Kanuni za Usafiri wa Anga kuhusu Mitambo na Vifaa vya Ndege za mwaka 2024 kama zilivyorekebishwa [Civil Aviation (Instruments and Equipment) Regulations, 2024];

   iv. Waraka wa Ushauri TCAA-AC-AWS001B kuhusu Ukubalifu na Usajili wa Ndege (Aircraft Acceptance and Registration).

Kwa taarifa zaidi tafadhali wasiliana kupitia:
airworthinessinspectors@tcaa.go.tz

Unahitaji Msaada?