MAJUKUMU YA MAMLAKA

(1) Majukumu ya Mamlaka ni:-

(a) Kutekeleza yafuatayo:

(i) kutoa, kuhuisha, kurekebisha na kufuta leseni za huduma za usafiri wa anga;

(ii) kuweka viwango vya bidhaa na huduma zinazodhibitiwa;

(iii) kuweka viwango vya masharti na hali za utoaji wa bidhaa na huduma zinazodhibitiwa;

(iv) kudhibiti viwango vya tozo na ada;

(v) kutunga kanuni kwa ajili ya kutekeleza madhumuni na masharti ya Sheria.

 

(b) Kufuatilia utendaji wa watoa huduma wanaodhibitiwa ikiwamo:

(i) viwango vya uwekezaji;

(ii) upatikanaji, ubora na viwango vya huduma;

(iii) gharama za huduma;

(iv) ufanisi katika uzalishaji na usambazaji wa huduma; na

(v) masuala mengine yanayohusiana na Mamlaka.

 

(c) Kuwezesha utatuzi wa malalamiko na migogoro.

(d) Kuchukua na kuendelea kutekeleza majukumu yaliyokuwa yakifanywa na Mamlaka iliyokuwapo awali.

(e) Kusambaza taarifa kuhusu masuala yanayohusiana na majukumu ya Mamlaka.

(f) Kushauriana na mamlaka nyingine za udhibiti au taasisi zinazotekeleza majukumu yanayofanana na yale ya Mamlaka ndani ya Jamhuri ya Muungano na nje ya nchi.

(g) Kusimamia utekelezaji wa Sheria.

(h) Kupanga, kuendeleza, kudhibiti na kukuza uendeshaji wa mfumo wa usafiri wa anga ulio salama, wenye ulinzi na ufanisi.

(i) Kusimamia usalama, ulinzi na uchumi wa sekta ya usafiri wa anga.

(j) Kuanzisha na kutekeleza Mpango wa Taifa wa Usalama wa Anga (State Safety Programme).

(k) Kuweka kiwango kinachokubalika cha usalama wa anga.

(l) Kuishauri Serikali kuhusu masuala yanayohusu usafiri wa anga.

(m) Kuratibu shughuli za utafutaji na uokoaji wa ndege.

(n) Kushughulikia vitendo haramu katika usafiri wa anga.

(o) Kuanzisha, kusimamia na kuendesha taasisi za mafunzo kwa ajili ya sekta ya usafiri wa anga.

(p) Kupanga, kuendeleza na kuandaa usimamizi salama, wenye ulinzi na ufanisi wa anga la Tanzania.

(q) Kutekeleza majukumu mengine yoyote yatakayokabidhiwa kwa Mamlaka chini ya Sheria hii au sheria nyingine yoyote.

 

MASHARTI YA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU

(2) Katika utekelezaji wa majukumu yake, Mamlaka haitatekeleza shughuli zake kwa namna inayokiuka makubaliano yoyote ya kimataifa ambayo Jamhuri ya Muungano ni mwanachama wake.

(3)Katika utekelezaji wa majukumu yake, Mamlaka haitatoa wala kufuta leseni ya kipekee (exclusive license) au leseni ya wajibu wa huduma kwa wote (universal service obligation license) bila kushauriana na Waziri.

(4)Licha ya masharti yaliyotangulia katika kifungu hiki, Waziri anaweza mara kwa mara, kadiri mazingira yatakavyohitaji, kutoa maelekezo kwa Mamlaka yenye tabia mahsusi au ya jumla kuhusu masuala maalumu yasiyohusiana na utekelezaji wa kazi za udhibiti, yanayotokea katika sekta yoyote, kwa madhumuni ya kuhakikisha utekelezaji bora wa sera, majukumu na uzingatiaji wa maadili ya utendaji wa Mamlaka.

(5) Maelekezo yoyote yatakayotolewa na Waziri kwa mujibu wa kifungu kidogo cha (4) yatakuwa kwa maandishi na yatachapishwa katika Gazeti la Serikali.

(6) Mbali na majukumu yake ya udhibiti, Mamlaka inaweza kutoa huduma za uongozaji wa ndege; isipokuwa haitatoa huduma za hali ya hewa ya anga (aeronautical meteorological services).

(7) Katika kutoa huduma za uongozaji wa ndege, Mamlaka itahakikisha kuwa kunakuwapo mgawanyo na uteng

Unahitaji Msaada?