Usimamizi wa Watoa Huduma za Uongozaji wa Ndege na Huduma za Hali ya Hewa kwa ajili ya Uongozaji ndege
Katika kuhakikisha uzingatiaji wa matakwa ya kikanuni yanayohusiana na utoaji wa huduma, mmiliki wa Cheti cha ANSP atapaswa:
Kila wakati kuthibitisha uzingatiaji wa kanuni zinazotumika; na
- Kuzingatia utaratibu na michakato yote iliyoainishwa katika Mwongozo wake.
- Kitengo cha Ukaguzi kitafanya ukaguzi wa usalama na tathmini za kina (audits) za miundombinu, huduma, nyaraka na kumbukumbu za Watoa Huduma za Uongozaji wa Ndege (ANSP) ili kuhakikisha kuendelea kuzingatia kanuni hizi. Ukaguzi wa usalama na tathmini hizo zitafanywa kwa mujibu wa programu za ufuatiliaji za mwaka zilizoidhinishwa.
Mwisho, na muhimu zaidi, Mamlaka inaendelea kuwa na mamlaka ya kuweka vikwazo vya uendeshaji au adhabu dhidi ya shughuli za mwenye cheti endapo kutakuwa na kutofuata matakwa ya uthibitisho au masuala yoyote ya usalama ambayo hayajatatuliwa.