Utaratibu wa Uthibitishaji wa AOC

Shirika lolote linalokusudia kuwa mtoa huduma za ndege aliyethibitishwa (Certified Air Operator) mwenye makao makuu ya shughuli ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa madhumuni ya usafiri wa anga wa kibiashara kwa umma, lazima liwe na Leseni halali ya Huduma za Usafiri wa Anga (Air Service License) na litapaswa kupitia utaratibu wa uthibitishaji wa hatua tano kama ifuatavyo:-

(a) Awamu ya 1 – Maombi ya Awali

(b) Awamu ya 2 – Maombi Rasmi

(c) Awamu ya 3 – Tathmini ya Nyaraka

(d) Awamu ya 4 – Maonesho ya Uwezo na Ukaguzi

(e) Awamu ya 5 – Uthibitishaji

 

Taratibu na maelekezo yanayohusiana na utaratibu wa uthibitishaji yamejumuishwa ndani ya Kanuni za Usafiri wa Anga kuhusu Uthibitishaji na Usimamizi wa Waendeshaji wa Ndege za mwaka 2017 kama zilivyorekebishwa [Civil Aviation (Air Operator Certification and Administration) Regulations, 2017] pamoja na Nyaraka za Mwongozo wa Kiufundi (Technical Guidance Materials – TGMs).

 

TANBIHI:

   1.   Hakuna shirika lenye makao makuu ya shughuli ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania litakaloruhusiwa kufanya shughuli za uendeshaji wa ndege kwa madhumuni ya usafiri wa anga wa kibiashara kwa umma bila kupata idhini kutoka kwa Mamlaka kama ilivyoainishwa katika Kanuni za Usafiri wa Anga kuhusu Uthibitishaji na Usimamizi wa Waendeshaji wa Ndege za mwaka 2017 kama zilivyorekebishwa.

   2.   Shughuli za uendeshaji wa ndege ambazo si za usafiri wa anga wa kibiashara kwa umma zimeainishwa kama Usafiri wa Anga wa Jumla (General Aviation) au Shughuli za Kazi za Angani (Aerial Work Operations). Kwa shughuli za usafiri wa anga wa jumla au kazi za angani zinazotumia ndege na helikopta zilizosajiliwa Tanzania, zitatumika Kanuni za Usafiri wa Anga kuhusu Uendeshaji wa Ndege – Usafiri wa Anga wa Jumla za mwaka 2024 kama zilivyorekebishwa [Civil Aviation (Operation of Aircraft – General Aviation) Regulations, 2024].

   3.   Kwa orodha ya hivi karibuni ya wamiliki wa Cheti cha Uendeshaji wa Ndege (AOC Holders), bofya hapa.

Unahitaji Msaada?