TANGAZO LA KUANZISHWA KWA DAFTARI LA UMMA
(Limetolewa kwa mujibu wa kifungu cha 56 cha Sheria ya Usafiri wa Anga (Sura ya 80 Toleo la 2023))
|
Kuanzishwa kwa Daftari la Umma |
1. Mamlaka inaanzisha Daftari la Umma kwa mujibu wa kifungu cha 56 cha Sheria. Daftari la Umma litaendeshwa na kusimamiwa kwa mujibu wa maelekezo yaliyotolewa katika Tangazo hili la Uanzishwaji. |
|
Mahali linapopatikana Daftari |
2. Daftari la Umma litapatikana kupitia tovuti ya Mamlaka. |
|
Uamuzi na taarifa zitakazohifadhiwa
|
3. (1) Pamoja na uamuzi na taarifa zinazotakiwa na Sheria kuwekwa katika Daftari la Umma kama ilivyoainishwa katika kifungu kidogo (2) hapa chini, Mamlaka mara kwa mara itaamua aina za uamuzi na taarifa zitakazowekwa katika Daftari la Umma na itamjulisha Waziri ipasavyo. (2) Daftari la Umma litakuwa na mambo yafuatayo:- (a) Kanuni za Maadili zilizopitishwa kama ilivyoainishwa katika kifungu cha 42(3) cha Sheria; (b) Sheria ndogo au kanuni zozote kama ilivyoainishwa katika kifungu cha 56(4)(b) cha Sheria; (c) Muhtasari wa uamuzi wowote wa Mamlaka unaoweka viwango vya bei au tozo kwa bidhaa au huduma zinazodhibitiwa kama ilivyoainishwa katika kifungu cha 56(4)(c) cha Sheria; (d) Uamuzi au taarifa nyingine yoyote ambayo Mamlaka inaweza kuamua kuchapisha katika Gazeti la Serikali kama ilivyoainishwa katika kifungu cha 56(4)(d) cha Sheria; (e) Programu ya mashauriano kama ilivyoainishwa katika kifungu cha 55(2) cha Sheria; (f) Ada zilizoainishwa za leseni na ada nyingine kama inavyotakiwa na kifungu cha 49(3) cha Sheria; na (g) Uamuzi au taarifa nyingine yoyote iliyoainishwa na sheria ndogo, taratibu, au kanuni. (3) Mamlaka haitaweka katika Daftari la Umma hati yoyote au sehemu ya hati ambayo ni ya siri kwa mujibu wa Taratibu zilizowekwa chini ya kifungu cha 57(2) cha Sheria. |
|
Muundo wa Daftari la Umma
|
4. Muundo wa Daftari umeandaliwa ili kutoa rejea ya haraka na rahisi kuhusu mada au taarifa ambazo watumiaji wanahitaji kuzipata. Daftari limegawanywa katika sehemu/sura na sehemu ndogo/sura ndogo zinazowaelekeza watumiaji mahali ambapo taarifa inayohusika zinaweza kupatikana. |
|
Usimamizi wa Daftari la Umma
|
5. (1) Ofisi ya Uhusiano kwa Umma ina wajibu wa kusimamia Daftari la Umma, hususani kuhakikisha upatikanaji wake kwa umma. (2) Daftari la Umma litakuwa na taarifa za sasa wakati wote. Uamuzi na taarifa zinazotakiwa kuonekana katika Daftari la Umma zitawekwa kwenye Daftari ndani ya siku saba za kazi tangu uamuzi au taarifa hizo kupatikana. (3) Mamlaka itaweka taratibu zitakazofuatwa katika kuweka au kurekebisha taarifa kwenye Daftari la Umma. |