CoA

Ili ndege yoyote iweze kuendeshwa ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (URT), inatakiwa kuwa na Cheti cha Ubora wa Ndege Kuruka (Certificate of Airworthiness – C of A) kilichotolewa na Mamlaka au cheti kinachotambuliwa kilichotolewa na nchi mwanachama wa Mkataba wa Chicago.

Kwa ajili ya kuomba Cheti cha Ubora wa Ndege Kuruka (C of A), fomu zifuatazo, kulingana na aina ya maombi yanayohusika yanapaswa kujazwa na kuwasilishwa kwa Mamlaka:-

i. Kwa ajili ya utoaji na uhuishaji wa Cheti cha Ubora wa Ndege Kuruka, Cheti  chenye katazo cha Ubora wa Ndege Kuruka (Restricted Certificate of Airworthiness), pamoja na Cheti cha Kusafirisha Ndege Nje ya Nchi (Export Certificate of Airworthiness), tumia nyaraka za udhibiti zifuatazo:

  • TCAA-AC-AWS002B
  • TCAA-AC-AWS002C
  • TCAA-AC-AWS002D

ii. Kwa kibali maalumu cha safari ya ndege (Special Flight Permit), tumia Fomu TCAA-AC-AWS004A pamoja na nyaraka husika zifuatazo:-

  • Bima ya ndege;
  • Leseni ya rubani;
  • Cheti cha Uwezo wa Ndege Kuruka (Certificate of Fitness for Flight – CFF).

 

Kwa mwongozo zaidi rejea nyaraka zifuatazo za kiudhibiti

i. Kanuni za Usafiri wa Anga kuhusu Ubora wa Ndege Kuruka za mwaka 2017, kama zilivyorekebishwa [Civil Aviation (Airworthiness) Regulations, 2017];

ii. Kanuni za Usafiri wa Anga kuhusu Mitambo na Vifaa vya Ndege za mwaka 2024, kama zilivyorekebishwa [Civil Aviation (Instruments and Equipment) Regulations, 2017];

iii. Waraka wa Ushauri TCAA-AC-AWS021C kuhusu ukubalifu wa kanuni za kigeni za ubora wa ndege kuruka kwa cheti cha aina ya ndege na taarifa za kina (Type Certificate na data sheet);

iv. Waraka wa Ushauri TCAA-AC-AWS002B kuhusu utoaji wa Cheti cha Ubora wa Ndege Kuruka;

v. Waraka wa Ushauri TCAA-AC-AWS003C kuhusu uhuishaji wa Cheti cha Ubora wa Ndege Kuruka;

vi. Waraka wa Ushauri TCAA-AC-AWS004D kuhusu Cheti chenye katazo cha ubora, Cheti cha ubora cha Kusafirisha Ndege Nje ya Nchi pamoja na kibali maalumu cha ndege kuruka.

vii. Tozo inayohusika kama ilivyoainishwa katika Waraka wa Taarifa za Anga Aeronautical Information Circular (AIC).

Kwa maelekezo zaidi tafadhali wasiliana nasi kupitia:
airworthinessinspector@tcaa.go.tz

 

Unahitaji Msaada?