TARATIBU ZA VIBALI VYA DRONI TANZANIA
1. Wasio Wakazi (Non-Residents)
Mtu yeyote anayesafiri kuja Tanzania akiwa na droni anatakiwa kuhakikisha anafanya yote yafuatayo:
- Kuomba Kibali cha Kuingiza Nchini (Import Permit)
(Bila kibali cha TCAA cha kuingiza nchini, droni itataifishwa itakapowasili mahali rasmi pa kuingilia nchini.) - Kusajili droni yako
- Kumsajili mwendeshaji wa droni (Rubani wa Droni)
- Kuomba Kibali cha Uendeshaji
Maombi hayo hapo juu lazima yafanywe na mwombaji angalau WIKI TATU kabla ya kuja Tanzania.
Maombi yote yanafanywa kupitia mfumo wetu wa mtandaoni, na ili kupata huduma hiyo mwombaji atatuma taarifa zifuatazo kupitia baruapepe yetu (drones@tcaa.go.tz):
- Jina kamili la mwombaji
- Baruapepe
- Namba ya simu yenye msimbo wa nchi
- Anwani ya makazi (Mtaa, Jiji na Nchi)
- Namba ya pasipoti
- Utaifa
- Aina ya droni na madhumuni ya matumizi
- Tarehe inayotarajiwa kuwasili
Baada ya kutuma taarifa hizo, mwombaji atasajiliwa na atapokea baruapepe kutoka TCAA yenye kiunganishi (link), jina la mtumiaji na nywila.
Tangazo Muhimu: Hakutakuwa na marejesho ya fedha iwapo mwombaji atashindwa kukamilisha maombi yote kwa wakati.
2. Wakazi (Residents)
Kwa wakazi wa Tanzania kuna makundi matatu:
- Wanaonunua droni nje ya nchi
- Wanaonunua droni ndani ya nchi
- Wauzaji/Wasambazaji
Wanaonunua droni nje ya nchi:
- Kuomba Kibali cha Kuingiza Nchini (Import Permit)
(Bila kibali cha TCAA cha kuingiza nchini, droni itataifishwa itakapowasili mahali rasmi pa kuingilia nchini.)
- Kusajili droni
- Kumsajili mwendeshaji wa droni (Rubani wa droni)
- Kuomba Kibali cha Uendeshaji
Wanaonunua droni ndani ya nchi:
- Kusajili droni
- Kumsajili mwendeshaji wa droni (Rubani wa droni)
- Kuomba Kibali cha Uendeshaji
Wauzaji/Wasambazaji:
- Kuomba Kibali cha Kuingiza Nchini (Import Permit)
(Bila kibali cha TCAA cha kuingiza nchini, droni itataifishwa itakapowasili mahali rasmi pa kuingilia nchini.)
Maombi yote yanafanywa kupitia mfumo wa mtandaoni na ili kupata huduma hiyo, mwombaji atatuma taarifa zifuatazo kupitia baruapepe yetu (drones@tcaa.go.tz).
Ikiwa droni ni kwa matumizi binafsi:
- Jina kamili la mwombaji
- Baruapepe
- Namba ya simu
- Anwani ya makazi (Mtaa, Wilaya na Jiji)
- Namba ya NIDA/Pasipoti
- Aina ya droni na madhumuni ya matumizi
Ikiwa droni ni kwa matumizi ya kampuni/shirika:
- Jina la kampuni/shirika
- Baruapepe
- Namba ya simu
- Anwani ya makazi (Mtaa, Wilaya na Jiji)
- Aina ya droni na madhumuni ya matumizi
Baada ya kutuma taarifa hizo, mwombaji atasajiliwa na atapokea baruapepe kutoka TCAA yenye kiunganishi, jina la mtumiaji na nywila.
Taarifa Muhimu: Ikiwa mkazi atauza droni kwa mtu mwingine, lazima aiarifu Mamlaka (TCAA).